Mgombea
ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa (32), akiwapungia
wananchi huku akiwa amebebwa alipowasili kwenye mkutano wa kampeni
katika Kijiji cha Mangalali, Kata ya Ulanda, Iringa Vijijini jana mchana. |
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba akiongoza msafara wa mgombea ubunge
wa Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa aliyebebwa walipowasili kwenye
mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Mangalali.
|
Mgimwa
akiungana na wanakijiji kucheza ngoma ya asili ya kabila la Wahehe
alipowasili kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Kibebe, Kata ya
Ulanda mchana leo.
|
Mchungaji
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Usharika wa Kalenga
Tosamaganga, Kisabugo Mkemwa akitoa mahubiri ya kumuombea Mgimwa
(kushoto) ili ashinde uchaguzi huo. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa
CCM, Nchemba. |
Mjumbe
wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Iringa, Aloyce Mgongolwa akisikiliza
kwa makini wakati Nchemba akihutubia katika mkutano huo wa kampeni
katika Kijiji cha Kibebe. |
Ofisa
Mwandamizi wa Mawasiliano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Gabriel
Athuman akinywa maji ya kisima ambayo aliyasifia kuwa ni matamu wakati
wa mkutano wa Kampeni za CCM Jimbo la Kalenga katika Kijiji cha Kibebe
Akina mama wakisikiliza kwa makini wakati Mgimwa akijinaji katika mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Kibebe leo mchana.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Joyce Msambatavangu akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kalenga, Mgimwa.
Aliyewahi
kuwa Mgombea ubunge Jimbo la Mbozi Mashariki kupitia Chadema, na Ofisa
wa Chadema Makao Makuu, Mwampamba akielezea jinsi alivyoamua kujiondoa
kwenye chama hicho bhaada ya kufanyiwa mabaya na uongozi wa Chadema
ambacho alidai hakifai wananchi kujiunga nacho.
No comments:
Post a Comment