Pages

Pages

Wednesday, March 12, 2014

Twanga Pepeta kuiacha Dar kwa wiki moja, kutembelea pia Mbamba Bay mkoani Ruvuma

Twanga Pepeta kuiacha Dar kwa wiki moja, kutembelea pia Mbamba Bay mkoani Ruvuma   

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya The African Stars, Twanga Pepeta, itakuwa nje ya jiji la Dar es Salaam kwa wiki moja, kutokana na kuwa na ziara ya kuinadi albamu yao ya Nyumbani ni Nyumbani, katika mikoa ya Njombe, Ruvuma na Mbeya kuanzia Machi 26 mwaka huu.
Kiongozi wa bendi ya Twanga Pepeta, Luiza Mbutu, akifanya mambo jukwaani katika moja ya maonyesho ya bendi yake.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa bendi hiyo, Hassan Rehani, alisema kuwa Machi 26 wataanza na shoo katika Ukumbi wa Turbo Hall, uliopo mkoani Njombe, wakati siku inayofuata watacheza na mashabiki wao Mbamba Bay, katika Ukumbi wa Bay live Social Hall.
Mwimbaji wa Twanga Pepeta, Kalala Junior, katikati akionyesha umahiri wake wa kucheza na jukwaa katika moja ya maonyesho ya bendi yake.
Alisema Machi 28 bendi yao itafanya shoo katika Ukumbi wa Serengeti, uliopo mjini Songea, wakati Machi 29 Twanga watatumbuiza City Pub, mjini Mbeya, huku Machi 30, wakifanya shoo High Class, uliopo mjini Tunduma.

“Hizi ni ziara maalum kwa ajili ya kwenda kuinadi albamu yetu na bendi yetu kwa ujumla, hivyo naamini wadau tutakuwa nao bega kwa bega.

“Tunaomba tushirikiane kwa nguvu mashabiki wetu ambao kwa kiasi kikubwa tumeamua kuwapelekea bendi yao ili wafurahie burudani za Twanga Pepeta,” alisema.

Kwa kuwa na ziara ya mikoani, sasa wapenzi wa bendi hiyo watalazimika kusubiri kwa siki moja kabla ya kuanza tena kuipata burudani ya Twanga Pepeta.

No comments:

Post a Comment