Pages

Pages

Wednesday, March 12, 2014

Simba wajitetea kwa mashabiki wao

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI wa klabu ya Simba, umesema kwamba kufanya vibaya katika mechi zake za Ligi Kuu hakutokani na timu hiyo kutoandaliwa vizuri, isipokuwa ni hali ya mchezo wa soka wenye matokeo ya kufungwa na kushinda.
Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga, pichani.
Simba kwa sasa inajiandaa na mechi yake dhidi ya Coastal Union, itakayopigwa Machi 23, katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni baada ya kuahirishwa baada ya kupangwa kufanyika leo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema timu yao imekuwa ikiandaliwa vizuri, lakini wanashindwa kupata matokeo mazuri ndani ya uwanja.

Alisema hali hiyo inasababishwa na ushindani uliopo kwenye ligi, hivyo ni wakati wa mashabiki kutochukizwa na suala hilo.

“Tunashindwa kupata matokeo mazuri uwanjani si kwasababu timu yetu haiandaliwi vyema kama wanavyosema baadhi yao.

“Hivyo tutaendelea na maandalizi yetu, tukiamini kuwa mechi ijayo dhidi ya Coastal Union, hapo Machi 23 baada ya kusogezwa mbele,” alisema.

Simba imeshindwa kuonyesha dhamira ya kunyakua taji msimu huu wa ligi, hivyo kuwapa wakati mgumu mashabiki wao.

No comments:

Post a Comment