Pages

Pages

Tuesday, March 11, 2014

Ridhwani achukua fomu za Ubunge Chalinze

 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Ridhwan Kikwete akionesha fomu aliyochukua ya kugombea ubunge jimbo la hilo kulia kwake ni Katibu wa CCM wa Wilaya ya Bagamoyo, Kongo Kamate na Mbunge wa viti maalum wa jimbo la Charinze Subira Mgalu.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhwan Kikwete akijaza fomu ya kugombea jimbo hilo.
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhwan Kikwete akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea jimbo hilo
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhwan Kikwete akiongozana na wanachama wa CCM kwenda kuchukua fomu fomu katika ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Wilaya ya Bagamoyo.

Na Mwandishi Wetu, Pwani
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhwan Kikwete jana alichukua fomu katika ofisi za msimamizi wa uchaguzi wilayani  Bagamoyo na leo anatarajia kurudisha fomu hiyo.

Akisindikizwa na mamia ya wanachama na mashabiki wa CCM wa jimbo la Chalinze na Bagamoyo, Ridhwani alimhakikishia  ofisa wa uchaguzi wa wilaya ya Bagamoyo Shija Andrew, kuwa atazingatia taratibu zote za uchaguzi na kutoendesha kampeni za matusi na vurugu.

Baada ya kuchukua fomu hiyo pamoja na nakala nyingine muhimu za uchaguzi aliongozana tena na mamia ya wafuasi wake kuelekea kwenye ofisi za CCM Bagamoyo ambapo alizungumza na waandishi wa habari.

Katika mazungumzo yake hayo Ridhwan alitaja vipaumbele vyake kwa kuleta maendeleo kwa wakazi wa Chalinze ambapo alisisitizia kuimarisha upatikanaji wa maji salama na ya uhakika, kuimarisha afya, elimu pamoja na kukuza ajira kwa vijana.
"Kama  mnavyofahamu kuwa Chalinze ni eneo ambalo linakabiliwa na changamoto nyingi kama vile maji, umeme na hata suala zima la ajira kwa vijana sasa pindi ambapo nikipata Ubunge kwangu mimi nitahakikisha kuwa napunguza kama sio   kumaliza kabisa tatizo hilo"alisema Ridhwan. Aliongeza kuwa "Mimi nimeguswa na changamoto mbalimbali zinazowakuta wakazi wa wilaya hii na kama ambavyo nilisema kuwa sikushinikizwa ila ni kwa matakwa yangu mwenyewe naona kabisa kuwa nipo katika hali na nguvu ya kushirikiana na wananchi kumaliza shida za Chalinze".

Ridhwan pia alisema kuwa atasaidia kutatua ugomvi wa mara kwa mara unaowakumba wakulima na wafugaji na kuwataka wakazi wa Chalinze kumchagua kwa kishindo. Wakati huo huo mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema Matayo Torongey akizungumza baada ya kuchukua fomu alisema kuwa anavyo vipaumbele vingi kimojawapo ikiwa ni kuinua maisha ya wakazi wa Chalinze.
Leo Ridhwan anatarajiwa kurejesha fomu za kugombea ubunge katika ofisi ndogo za uchaguzi.

No comments:

Post a Comment