Pages

Pages

Tuesday, March 11, 2014

TFF waiwekea mikakati Taifa Stars

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini (TFF), limesema kwamba limejipanga kumpata kocha wa timu ya Taifa, Taifa Stars, ili aanze mikakati ya kuinoa timu hiyo.


Stars imerejea nyumbani huku ikishindwa kuwatambia wenyeji wao Namibia, baada ya kutoka sare ya bao 1-1, katika mechi ya Kimataifa ya kirafiki.


Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa TFF, Boniface Wambura, alisema kuwa mchakato huo wa kumasaka kocha mpya wa Stars umeshaanza, wakiwa na imani ya kumpata haraka iwezekanavyo.


Alisema kocha Salum Madadi alikuwa wa muda kwasababu ana majukumu mengine ya kiutendaji ndani ya TFF, hivyo wanaamini hilo litafanikiwa.


“Tunahitaji kuwa na kocha bora na timu yenye nguvu zaidi, hivyo naamini kinachofanyika sasa ni kupigania uwezekano wa kupatikana mbadala wa Madadi.


Hata mipango ya kuiendeleza na kuiandaa zaidi timu yetu ya Taifa itafanikiwa endapo benchi la ufundi litasimama imara baada ya kukamilisha mchakato wa upatikanaji wake,” alisema Wambura.


Ajira ya kocha wa Stars, Kim Poulsen ilifikia ukingoni, hivyo kulazimika TFF kumteua Madadi kukaimu nafasi yake kwa ajili ya mechi dhidi ya Namibia.

No comments:

Post a Comment