Pages

Pages

Monday, March 10, 2014

Mwinjuma Muumini apiga hesabu za mikoani



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI mahiri wa muziki wa dansi nchini, Mwinjuma Muumini (Kocha wa Dunia), amesema anatamani awe na bendi imara Kahama, mkoani Shinyanga, ili kukuza soko la muziki huo hapa nchini.

Akizungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Muumini alisema bendi nyingi zimejikita maeneo ya jiji la Dar es Salaam, hivyo atamani kuwa na bendi maeneo ya Shinyanga.

Alisema anamini akifanikiwa juu ya hilo, mambo yatakuwa mazuri kwa kuona mikoani kunaanzishwa bendi imara na zenye ushindani wa aina yake.

“Bendi nyingi zimeendelea kuzaliwa katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam, hivyo wakati mwingine natamani nigeukie huko ili kuleta mfumo wa zamani wa mikoa kuwa na bendi imara na kuukuza muziki wetu.

“Naamini jambo hilo linaweza kuwa na tija kwa kiasi kikubwa katika maisha ya muziki wa dansi, hasa maeneo ya wilaya Kahama, mkoani Shinyanga, ambapo kumechangamka,” alisema Muumni.

Muumini kwa sasa hana bendi yoyote anayofanyia kazi, baada ya kuvunja mkataba wake katika bendi ya Victoria Sound, inayojulikana kama Malaika bendi, ikiwa chini ya Christian Bellah.

No comments:

Post a Comment