Pages

Pages

Monday, March 10, 2014

Kibadeni aipigania Ashanti ili isishuke daraja



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Kocha Mkuu wa timu ya Ashanti United, Abdallah Kibadeni, amesema
kuwa malengo yake makubwa kwa sasa ni kuhakikisha kuwa anapigania ili timu yake isiweze kushuka daraja.

Timu hiyo ilitoa sare ya bila kufungana Jumamosi iliyopita katika Uwanja wa Mkwakwani walipocheza na Wagosi wa Kaya, Coastal Union yenye maskani yake mjini Tanga.
Alisema kuwa ingawa timu yao ilicheza kwenye kiwango cha chini dhidi ya Coastal, lakini kwa sasa wameweka juhudi nzito kukabiriana na suala hilo kwa ajili ya kuinusuru klabu hiyo inayosua sua.

"Tunashukuru kwasababu tulipata pointi moja dhidi ya Coastal Union, ila juhudi zetu kwa pamoja ni kupigania Ashanti isishuke daraja, ukizingatia kuwa kumekuwa na ushindani mkubwa na harakati za kila timu kusaka ushindi," alisema.

Alisema ligi kuu soka Tanzania bara mzunguko wa pili ni ngumu kwa kusema matarajio yake ni kuhakikisha wanafanya vziuri kwenye mechi zao zinazofuata kwani hicho ndio kitu pekee ambacho kitampa ridhaa ya wao kuendelea kubaki kwenye mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment