Pages

Pages

Monday, March 10, 2014

Bunge la Katiba lazidi kuwaka moto, William Lukuvi ataka aendelee kuzomewa, laahirishwa hadi saa 10 jioni



Na Mwandishi Wetu, Dodoma
KAMA ilivyotarajiwa na wengi, Bunge la Katiba limeahirishwa tena mchana wa leo hadi hapo saa 10 jioni baada ya mvutano wa wajumbe na Kamati ya Kanuni kuendelea. Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hilo, Pandu Ameir Kificho, aliwataka wajumbe kujiandaa hadi sioni ili wapitishe kanuni hizo.

William Lukuvi, Mjumbe wa Bunge la Katiba
Awali mjumbe wa Bunge hilo, David Kafulila, alimtaka mwenyekiti wao kuhakikisha kuwa Bunge hilo linasitishwa hadi mvutano wao utakapomalizika ili kuokoa posho zinazoendelea kutafutwa bila kufanyiwa kazi.

Wakati hayo yanaendelea, kila mjumbe alikuwa akifanya vituko, ikiwamo kuwasha kipaza sauti na kuzungumza bila kupewa ruhusa na mwenyekiti wake.

Mjumbe mwingine wa Bunge hilo, William Lukuvi, aliwajia juu baadhi ya wajumbe wengine akisema kuwa wamekwenda Bungeni kuzomea. “Naomba niseme kitu kimoja, wengine hatuogopi kuzomewa, tumeshazomewa sana hivyo hatuogopi.

Endeleeni kuzomea lakini lazima niseme maana wanaozomea ni wale wale wa siku zote, hivyo katika hili lazima tujuwe kuwa wananchi wanatushangaa kwasababu hatufanyi kazi iliyotuleta hapa,” alisema Lukuvi.

Kauli yake iliibua zogo zito, hivyo mwenyekiti wa muda kuwataka wajumbe kuwa makini na kuacha kuzungumza bila kupewa ruhusa.

No comments:

Post a Comment