Pages

Pages

Wednesday, March 05, 2014

Logarusic ataka wachezaji waongeze umakini



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KOCHA Mkuu wa Simba, Zdravok Logarusic, amewataka wachezaji wake kutumia vizuri nafasi wanazopata ili washinde katika mechi yao dhidi ya Ruvu Shooting, mchezo unaotarajiwa kupigwa kesho katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Logarusic alisema timu yote inahitaji ushindi katika mechi yao hiyo, hivyo jambo kubwa ni kuona vijana wake wanakuwa makini zaidi uwanjani.

“Tumepoteza pointi muhimu katika mechi iliyopita kwasababu ya wachezaji kutotumia ipasavyo nafasi za wazi wanazozipata, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limetugharimu.

“Naamini wakati huu wachezaji wote wanafahamu jambo gani muhimu wanapaswa kufanya uwanjani kwa ajili ya kuwapatia maatokeo mazuri, maana mpira ni mchezo wa makosa,” alisema.

Alisema kuwa kila mchezaji anaweza kufunga anapokuwa katika nafasi mzuri ya kufunga na kuhakikisha nafasi tatu za wazi wanazozipata moja wapo wanaibuka na ushindi.

Simba itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu za kichapo cha mabao 3-2 dhidi ya JKT Ruvu, uliochezwa Jumapili iliyopita katika uwanja wa Taifa, mechi iliyowasononesha mashabiki wao.

No comments:

Post a Comment