Pages

Pages

Saturday, March 08, 2014

Kampeni za Uchaguzi Jimbo la Kalenga zaendelea kushika kasi

 Mwenyekiti wa Chadema katika kijiji cha Wangama jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, Fred Mgata (kulia) akikabidhi kadi ya chama hicho kwa Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga, baada ya kutangaza kuhamia CCM, kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa CCM jimboni humo, leo. Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wapo wanachama wengine 50 alioambatana nao kutoka Chadema. Kijiji hicho cha Wangama ndiko anakotoka mgombea wa Chadema katika uchaguzi huo, Grace Tendega.
 Mwanamke, mkazi wa Kijiji cha Wangama akimpongeza Fred Mgata baada ya uamizi wake wa kuhamia CCM kutoka Chadema.
 Mgombea wa CCM jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa akimshukuru Mwenyekiti wa Chadema Kijiji cha Wangama baada ya kutangaza kuhamia CCM leo.
 Wananchi wsa Kijiji cha Wangama wakiishangilia CCM kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika kijiji hicho leo.
 Mgombea wa CCM Godfrey Mgimwa akiwashukuru kina mama baada ya mkutano wake wa kampeni uliofanyika Kijiji cha Wangama leo.
 Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Seif Shabani Mohammed akihutubia mkutano wa kampeni za CCM katika kijiji cha Ikuvilo, jimbo la Kalenga leo.
 Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Arusha Mjini, Rehema Mohamed akisisitiza jambo alipohutubia mkutano wa kampeni za CCM katika jimbo la Kalenga, leo.
Kada wa CCM kutoka Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa CCM, Juliana Shonza akisalimia wananchi katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo, Kijiji cha Ikuvilo.

No comments:

Post a Comment