Pages

Pages

Friday, March 07, 2014

DC Muhingo alipozuru Chumba cha habari cha New Habari 2006 Ltd

Mkuu wa Wilaya Handeni, mkoani Tanga, Muhingo Rweyemamu, kulia akipitia gazeti la Michezo la Bingwa, akiwa sambamba na Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda katikati, pamoja na mke wake Fatuma Waziri kushoto. 

New Habari ni wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Bingwa, Dimba, Rai na The African, wakiwa na maskani yao Sinza Kijiweni, jijini Dar es Salaam. DC Muhingo alitumia muda huo alipotembelea chumba cha habari hicho na kujadili mambo mbalimbali na Kibanda. 

DC Muhingo ni kama vile ametembelea nyumbani kwake kutokana na taaluma yake ya habari, huku akiwahi kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo ambapo nafasi hiyo ipo chini ya Kibanda kwa sasa. Picha na Jumanne Juma.


No comments:

Post a Comment