Pages

Pages

Sunday, March 09, 2014

DC Handeni apigia hesabu soka la shule za sekondari



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKUU wa Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, Muhingo Rweyemamu, amesema kwa sasa ana mikakati kabambe kuhakikisha shule zote za sekondari wilayani humo, zinashiriki mashindano ya mpira wa miguu ili kuendeleza vipaji vyao.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, pichani.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Rweyemamu alisema hali hiyo inasababishwa  na wingi wa vijana wenye uwezo wa kucheza soka, ila wanakosa misingi imara ya kuwaendeleza.

Alisema baada ya kuwafuatilia kwa makini vijana mbalimbali, amebaini ili iwe na tija, kuna ulazima wa kuhakikisha kuwa watoto wanaanzia hatua ya chini kabisa kucheza soka.

“Nitazungumza na wenzangu ili kuhakikisha kuwa nia yangu ya kuendesha mashindano ya vijana kwa kupitia shule zote za sekondari inafanikiwa kwa vitendo.

“Naamini mpango huu utakuwa na tija kwa kiasi kikubwa, ukizingatia kuwa tukiweza hivyo, wanafunzi wetu watakuwa na mahala kwa kuonesha vipaji vyao,” alisema.

No comments:

Post a Comment