Pages

Pages

Saturday, February 08, 2014

Yanga wakata mpapai kwa shoka, baada ya kuwatandika vibonde Komorozine bao 7-0 Uwanja wa Taifa

YANGA leo imeanza vyema michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kuitandika bila huruma timu kibonde ya nchini Comoro, inayoitwa Komorozine, iliyotua Tanzania juzi. Mara baada ya kuwasili, viongozi wa timu hiyo, walizungumzia mchezo wao.
Mwandishi Saada Akida, akiandika baadhi ya vitu vilivyokuwa vinazungumzwa na wageni wa Yanga, timu ya Komorozine ya nchini Comoro ambao leo wamejikuta wakipigwa bao 7-0 katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Anayefuata mwenye shati jeupe ni Kambi Mbwana, akiwa sambamba na Bernad Mwalala, nyota wa zamani wa klabu ya Yanga.

Hata hivyo walionyesha woga kwa Yanga, huku wakishikwa na presha juu ya majina kadhaa ya Yanga, akiwamo Mrisho Ngassa, ambaye leo amefunga bao tatu kwa mguu wake mwenyewe. Wengine waliofungia Yanga leo ni pamoja na Nadir Haroub Cannavaro na Didier Kavumbagu. Habari zaidi juu ya mchezo huo zitakuja kwa urefu.

Mara baada ya mechi hiyo kumalizika, baadhi ya wadau waliizungumzia mechi hiyo kuwa Yanga wamejaribu kuukata mpapai kwa kutumia shoka, yani ni kutokana na ulege lege wa wachezaji hao wa Comoro wanaofungwa bao nyingi kila mwaka.

 

No comments:

Post a Comment