Pages

Pages

Tuesday, February 04, 2014

Waziri Mukangara awafunda maafisa mawasiliano serikalini

Waziri Habari Utamaduni na Michezo, Dkt Fennellah Mukangara, akizungumza katika kikao cha Maafisa Habari na Mawasiliano wa serikalini, mkoani Tanga. 
Na Oscar Assenga, Tanga.

WAZIRI wa Habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo Dokta Fenella Mukangara ametoa wito
kwa Maafisa Mawasiliano wa Serikali kwenye wizara, Idara na Taasisi za serikali kuendelea kujifunza kwa weledi mambo mbalimbali yatakayosaidia kuleta tija katika kutekeleza majukumu yao ya kusimamia mawasiliano kwenye maeneo yao ya kazi.



Mukangara ametoa wito huo jana wakati wakifungua kikao cha kazi cha maafisa mawasiliano kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini kilichofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
    
NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA HABARI VIJANA,UTAMADUNI NA MICHEZO PROF.ELISANTE OLE GABRIEL AKIZUNGUMZA KWENYE KIKAO HICHO KABLA YA KUMKARIBISHA WAZIRI.

Amesema maafisa hao wamepewa jukumu kubwa la kuiwezesha serikali kuipitia ofisi zao kufanya mawasiliano na umma kupitia vyombo vya habari kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sera na miradi inayotekelezwa na serikali yenye lengo la kustawisha maendeleo kwa watanzania.


Amesema kimsingi wasemaji wa wizara ,idara na taasisi wao ndioa wasemaji wakuu badala ya watendaji wakuu wa sehemu zenu za kazi hivyo serikali inatimiza wajibu wake wa kutoa haki ya msingi ya wananchi kupata habari hususani zinazohusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali serikalini.
 

Waziri huyo amesema kikao hicho kimebeba kauli mbiu isemayo "Matumizi ya mitandano ya Tehama na mitandao katika kuimarisha mawasiliano ya serikali kwa umma  ambapo amewaasa washiriki kutumia fuksa hiyo ya kuwepo mitandao ya kijamii ili kukidhi kiu ya jamii ya kupatiwa taarifa mbalimbali za kuelimishwa na kuburudishwa.

No comments:

Post a Comment