Pages

Pages

Tuesday, February 04, 2014

Kigoma yajidhatiti mashindano ya masumbwi

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KOCHA wa timu ya ngumi  Mkoa wa Kigoma, Juma Lesso amesema timu yake ya mkoa imekuja kamili kwa ajili ya mashindano ya wazi yatakayoanza Februari 5 katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Lesso alisema kuwa ni mara yao ya kwanza kwa timu ya Mkoa wa Kigoma kushiriki mashindano makubwa ya ngumi.
Alisema kuwa wameweka kambi yao Kawe, ikiwa ni baada ya kutoka Mabibo,wakiwa na lengo la kuhakikisha kuwa mambo yao yanakuwa mazuri.
“Tunamshukuru Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu Issa Machibya, kuhakikisha kuwa tunashiriki katika mashindano haya kwa mara ya kwanza.
“Tunaamini kuwa kila kitu kitakwenda vizuri na vijana wetu kufanya mambo ya maana katia mashindano haya yenye tija kwenye mchezo wa masumbwi,” alisema.
Kufanyika kwa mashindano hayo ya wazi ya ngumi inaweza kuwa silaha ya kufanikisha kwa vitendo mchezo huo uliokuwa unatamba hapa nchini.

No comments:

Post a Comment