Pages

Pages

Wednesday, February 05, 2014

Majeruhi waongezeka Azam fc

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WAKATI wapinzani wa timu ya Azam katika mashindano ya Kombe la Shirikisho, Ferroviario Da Beira ya Msumbiji ikiwasili leo, wachezaji wengine wawili wameongezeka kuwa majeruhi katika kikosi hicho cha wauza ice cream wa Azam.

Wachezaji hao wawili waliongezeka ni pamoja na Ismail Gambo na Haji Samir, ambao sasa wataungana na majeruhi wenzao watatu, akiwamo John Bocco, Farid Malicky na Waziri Salum, ambao wote kwa pamoja watakosa mechi dhidi ya Ferroviario, mechi itakayopigwa Jumapili katika Uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Azam, Jafar Idd, alisema kuwa wachezaji hao wote wapo chini ya uangalizi wa daktari, hivyo watakosa mechi hiyo muhimu kwa timu yao inayoanza kuungwa mkono na Watanzania wengi.

“Tunaingia katika mchezo muhimu mno kwetu, huku tukikosa wachezaji watano ambao ni majeruhi na baadhi yao watalazimika kufanyiwa vipimo vikubwa zaidi.

“Tunaamini Mungu atakuwa upande wetu kwa kuhakikisha kuwa tunaanza vyema kwa kuibuka na ushindi dhidi ya wapinzani wetu hao wa Msumbiji,” alisema Idd.

Azam katika mchezo wake wa juzi dhidi ya timu ya Kagera Sugar iliweza kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0, hivyo kutangaza kiwango kizuri kabla ya kuanza patashika ya mashindano ya Kimataifa ya Kombe la Shirikisho.

No comments:

Post a Comment