Pages

Pages

Wednesday, February 05, 2014

Yanga waweka kambi Bagamoyo kuwawinda Comorizeni

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MABINGWA wa Tanzania Bara ambao ni wawakilishi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga, imeingia kambini rasmi jana mjini Bagamoyo, kwa ajili ya kujiwinda na mchezo wao dhidi ya Comorizeni ya Comoro, utakaochezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, pichani.
Yanga imeingia kambini katika hoteli ya Kilomo, mjini Bagamoyo, huku wakiwa na matumaini makubwa ya kuanza vyema katika michuano hiyo ya Kimataifa.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema kuwa timu yao ipo katika hali nzuri, huku wakiwa na shauku kubwa ya kufika mbali katika michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

“Tunashukuru kwa kwa kupata ushindi wetu dhidi ya timu ngumu ya Mbeya City, ambapo sasa vijana wapo imara na wameingia tena kambini kwa ajili ya Comorizeni.

“Ingawa wanasema Comorizeni si timu ngumu, ila bado haiwi sababu ya Yanga kubweteka katika mechi hiyo kwasababu siku zote mpira unahitaji maandalizi kama unahitaji ushindi,” alisema.

Wakati inajiandaa na mzunguuko wa pili wa Ligi ya Tanzania Bara, Yanga iliweka kambi yake nchini Uturuki ambapo walicheza mechi kadhaa za kirafiki kwa ajili ya kujiandaa vyema, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limewaweka katika hali nzuri.

No comments:

Post a Comment