Pages

Pages

Sunday, February 09, 2014

Endru G achekelea Umenibamba


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

MKALI wa muziki wa kizazi kipya, Andrew George, maarufu kama Endru G, pichani chini, amewashukuru wadau wa muziki kuupokea kwa shangwe wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Umenibamba’, unaofanya vyema katika vituo vya redio na televisheni.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Endru G alisema wimbo huo umepokewa kwa shngwe na mashabiki wake, ambapo video yake aliitengeneza nchini Kenya, chini ya Kampuni ya Apex.


Alisema anaamini ni mwendo mzuri kuelekea kwenye mafanikio ya juu zaidi katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya, maarufu kama Bongo Fleva.

“Huu ni wakati wa kuendelea kupigania maendeleo ya juu zaidi katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya, ambapo kwa upande wangu sina shaka kuwa mashabiki wangu wananiunga mkono.


“Wimbo wangu wa Umenibamba umeendelea kufanya vyema katika kona mbalimbali, ambapo video yake niliitengeneza nchini Kenya, ingawa kampuni iliyotengeneza ni kutoka Tanzania, baada ya kusafiri wote huko kwa ajili ya kazi hiyo,” alisema.


Msanii huyo aliwahi kutamba na nyimbo kadhaa, ukiwamo ule wa Scora aliyoimba sambamba na nyota mwingine wa Bongo Fleva, Barnabas.

No comments:

Post a Comment