Pages

Pages

Sunday, February 09, 2014

Simba yapigwa 1-0 na Mgambo Shooting, Azam FC waanza kwa ushindi mbele ya Ferroviario ya Msumbiji Kombe la Shirikisho



MABINGWA wa zamani wa Tanzania Bara, Simba SC, imeonja joto ya jiwe baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Wanajeshi wa wilayani Handeni mkoani Tanga, Mgambo Shooting, mechi iliyopigwa leo katika Uwanja wa Mkwakwani, mjini hapa.

Bao hilo la pekee liliwekwa kimiani na Maganga Fully, dakika ya 29, akimalizia kazi nzuri kutoka kwa Peter Mwalyunzi, bao lilipokewa kwa hisia chungu mbele ya mashabiki wa Simba, ikiwa ni mwendelezo wa Ligi ya Tanzania Bara inayoendelea kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali.

Nayo Azam leo ilifanikiwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya wageni wao Ferroviario, katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho uliopigwa kwenye Uwanja wa Chamaz, uliopo Mbagala, jijini Dar es Salaam.

Bao hilo lilifungwa na  Kipre Tchetche kwenye dakika ya 42, ikiwa ni baada ya mvutano mkubwa kutoka kwa wapinzani wao, akitumia vyema pasi ya Brian Umony aliyopigwa kwa kichwa.

No comments:

Post a Comment