Pages

Pages

Saturday, January 04, 2014

Waendesha bodaboda wilayani Kilindi waomba kupewa leseni

Na Mwandishi Wetu, Kilindi
WAENDESHA Boda Boda wilayani Kilindi mkoani Tanga wameiomba Mamlaka ya Mapato mkoani Tanga (TRA), kuwapeleka wilayani humo huduma ya upatikanaji wa leseni kutokana na vijana wengine kutokuwa nazo hali inayochangiwa na kutokwepo kwa ofisi inayoshughulika na masuala hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, DC Selemani Liwowa, pichani.
Kilio hicho kilitolewa hivi karibuni na wananchi wa kata ya Kwediboma wilayani hapa wakati wakizungumza ambapo walisema kwa muda mrefu wamekuwa wakiikosa kitendo ambacho kinawalazimu kusafiri mpaka Tanga mjini ili kufuata huduma hiyo.
Evarist Mosha mkazi wa kata hiyo na dereva wa bodaboda alisema kukosekana kwa huduma hiyo wilayani humo serikali inakosa mapato kutokana na waendesha boda boda  wengi kutokuwa na leseni.
Akizungumzia suala hilo, Mkuu wa wilaya ya Kilindi, Suleiman Liwowa alisema ni kweli katika wilaya hiyo hakuna ofisi za mamlaka ya mapato (TRA) na kutaka uwekwe utaratibu ambao utawafikia wananchi na endapo watakubaliana nao wataweka mazingira mazuri ya upatikaji ofisi.

No comments:

Post a Comment