Pages

Pages

Sunday, January 05, 2014

Jahazi kukamua Morogoro Januari 31



KUNDI bingwa la miondoko ya mwambao, Jahazi Modern Taarab litaanza kutambulisha nyimbo zake mpya mwishoni mwa mwezi huu ambapo mji wa Morogoro utakuwa wa kwanza kupata uhondo huo.
Wakali wa Jahazi Modern Taarab, pichani.
Jahazi watafanya onyesho maalum mjini humo Ijumaa ya Januari 31 ndani ya ukumbi wa Tanzanite Complex.
Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa Jahazi kupiga ndani ya ukumbi huo uliofunguliwa kiasi cha mwaka mmoja uliopita.
Kwa mujibu wa mratibu wa onyesho hilo Warda Makongwa wa Planet FM ya mjini humo, wameamua kuandaa onyesho hilo kufuatia maombi ya mashabiki wengi waliotaka Jahazi nayo ibishe hodi ndani ya Tanzanite Complex.
Warda amesema Jahazi halitaenda hivi hivi bali litaandamana na nyimbo mpya kabisa ambazo hazijawahi kusikika hapo kabla.
Amefafanua kuwa nyimbo hizo ni sehemu ya maandalizi ya albam mpya ijayo ya Jahazi Modern Taarab inayoongozwa na Mfalme Mzee Yussuf.


No comments:

Post a Comment