Pages

Pages

Saturday, January 04, 2014

Cheka ashangazwa na sera ya michezo Tanzania



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA wa ngumi za kulipwa hapa nchini, Francis Cheka, amesema kwamba hakuna bondia anayeweza kupiga hatua kama wadau wa masumbwi wataendelea kuweka akili zao katika mchezo wa mpira wa miguu.
Francis Cheka, pichani.
Hayo yamekuwa malalamiko ya Cheka ya mara kwa mara, jambo linaloonyesha kuwa suala hilo limeshika hatamu katika juhudi zinazoangusha mchezo wa masumbwi.

Akizungumza jana kwa njia ya simu akitokea mkoani Morogoro, Cheka alisema kuwa serikali kwa kupitia wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo imeweka akili zao kwenye soka.

“Unaponiambia mimi najiandaa vipi na ngumi za kimataifa inaniuma kwasababu hakuna anayeweza kusonga mbele kama mfumo wetu utakuwa umeoza kwa kiasi kikubwa.

“Naomba wadau wa masumbwi wote wahakikishe kuwa maendeleo ya michezo ukiwamo wa ngumi unapiga hatua,” alisema Cheka.

Cheka ni miongoni mwa mabondia wanaofanya vizuri katika mchezo wa masumbwi hapa nchini, huku akifanikiwa kuibuka na ushindi kwa mapambano mengi nchini.

No comments:

Post a Comment