Pages

Pages

Saturday, January 18, 2014

Simba na Mtibwa hapatoshi leo uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MABINGWA wa zamani wa Tanzania Bara, Simba SC, leo wanashuka katika Dimba la Uwanja wa Taifa kuvaana na Wakata miwa wa Mtibwa Sugar, yenye maskani yao Turiani mkoani Morogoro.


Picha hii ikiwaonyesha wachezaji wa Simba, wakijinoa.
Mchezo huo wa kirafiki unaosubiriwa kwa hamu na mashabikiwa kandanda, unafanyika kama sehemu ya kuviandaa vikosi hivyo vimavyojiandaa pia na patashika ya Ligi ya Tanzania Bara, ambapo hatua ya mzunguuko wa pili inaanza Januari 25 mwaka huu.


Mchezo huo utakaoanza saa 10 jioni, unafanyika huku Simba wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kushindwa kutwaa taji la Kombe Mapinduzi lilomalizika hivi karibuni visiwani Zanzibar.


Maandalizi ya mchezo huo yamekamilika, huku makocha wa pande zote mbili wakitambiana kuwa wote wataonyesha soka safi na lenye kusisimua mashabiki wa kandanda Tanzania.


Kocha wa Simba, Zdravko Lagarusic, alitamba kuwa kikosi chake kitaonyesha soka safi kwa ajili kuwapatia burudani mashabiki wao.


“Kikosi changu kipo vizuri na mazoezi tuliyofanya wiki nzima yamenipa jeuri ya kupata ushindi dhidi ya wapinzani wetu hao,”alisema


Naye Mack Mexime aliwahakikishia wadau wa Mtibwa Sugar kuwa ushindi mbele ya Simba ni lazima, ingawa wanacheza mechi ya kirafiki.

No comments:

Post a Comment