Picha mbalimbali zinaonyesha historia nzuri ya Tanga.
Hassan Abdallah na Andrew Kizenga Shundi
MBELWA, Chifu wa Wazigua mkoani Tanga, ndiye aliyekuwa mtawala wa jadi
wa kwanza kutia saini mkataba na Dk. Karl Peters na kusababisha mkoa wa
Tanga na eneo la bahari ya Hindi kutawalika na kuwa koloni la
Kijerumani…………….ENDELEA..
TUWAKUMBUKE MASHUJAA WETU WA TANGA!
CHILO MWANA MACHAU na wenzake...katika miaka 1812..1830 kiliibuka mashujaa waliowapinga" WAJERUMANI ..WAKORONI"
shujaa wa Kizigua aliye Leta sifa kubwa na nikati ya mashujaa wa
kizigua ambae aliupinga kwa nguvu zote ..utawara au uingiaji wa
WAJERUMANI
"chiro mwanamachau " na wenzie walipo bainika kuwa wao ni kikwazo kwao waliwaua kwa kuwanyonga maeneo ya mjesani huko Tanga.
si hilo tuu Bali wajerumani walitoa tishio kwa wazigua endapo
wataendelea kuwapinga utawala wao watawanyonga kama walivyo wanyonga
wakina chilo mwana mchau na wenzake hii ni hadibhi fupi ya mashujaa wa
kizigua.
Bwana Heri bin Juma alikuwa sultani wa Saadani
iliyokuwa bandari ya biashara kwenye mwambao wa Bahari Hindi Tanga
katika Tanzania kaskazini-mashariki tangu
miaka ya 1870.
Mtawala wa Saadani
Alitawala chini ya Sultani wa Zanzibar kama mkubwa wake lakini akafaulu
kutetea nafasi yake kama sultani aliejitegemea. 1882 aliweza kushinda
jeshi la Sultani Sayyid Bargash aliyetaka kutawala Saadani moja kwa
moja. Saadani kama miji mingine ya pwani ilifaidika na biashara ya
Wazungu walioleta bidhaa na kulipa ushuru. Alielewana vema nao.
Kuja kwa Wajerumani
1886 Sultani Sayyid Khalifa wa Zanzibar alikodi eneo lake katika
Tanganyika bara kwa Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki. Bwana
Heri pamoja na viongozi wengine aliona amesalitiwa na Sultani hakuwa
tayari kukubali utawala wa Wajerumani. 1888
Vita ya Abushiri
Bwana Heri aliunga mkono na upinzani wa Abushiri dhidi ya Wajerumani
akipata usaidizi wa makabila wa eneo lake hasa WAZIGUA. Akiwemo shujaa
maarufu wa kizigua aliyejulikana kwa jina la Senkondo Mwechiwa,
Alishambuliwa na kiongozi Mjerumani Hermann von Wissmann aliyekuwa na
silaha za kisasa akapaswa kuacha kambi yake Saadani tar. 6 Juni 1889.
Aliendela na vita ya msituni. Baada ya kushambuliwa tena na jeshi la
Wajerumani katika Januari na Machi 1890 uwezo wake ulikwisha. Sayyid
Khalifa aliwasiliana naye na Wissmann akatayarisha kujisalimisha kwake
tar. 6 Aprili 1890. Wissmann aliyemheshimu Bwana Heri hakumwua kama
Abushiri bali akamwambia kujenga Saadani upya.
Upinzani wa
wenyeji na utawala wa KIZIGUA ulishindwa lakini ulisababisha mwisho wa
utawala wa kampuni iliyoshindwa kukandamiza uasi wa Waafrika. Serikali
ya Ujerumani iliona haja ya kungilia kati na kuchukua utawala wa Afrika
ya Mashariki ya Kijerumani mkononi mwaka kama koloni ya serikali ya
Ujerumani.
Mwisho wake
Mwaka 1894 alijaribu kwa
kushirikiana na utawala wa kizigua tena kupambana na Wajerumani lakini
alishindwa kwa mara ya pili. Akaondoka bara kwenda Zanzibar alipokufa
baadaye.
KUINGIA KWA WAZIGUA SOMALIA
Asili ya Wazigua
waishio Somalia: pamoja na asili fupi ya Wazigua,baada ya Mjerumani
kuweza kutawala eneo la ukanda wa bahari ya Hindi na maeneo ya Tanga
hali hii ilipelekea………………………………..INAENDELEA
No comments:
Post a Comment