Pages

Pages

Saturday, January 18, 2014

CCM Handeni watema cheche Uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji



Na Mwandishi Wetu, Handeni
CHAMA Cha Mapinduzi CCM wilayani Handeni, mkoani Tanga, kimepania kuhakikisha kuwa hakuna chama chochote cha upinzani kinachoweza kutamba katika Uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji utakaofanyika mapema mwaka huu.



Mwenyekiti wa CCM wilayani Handeni, mkoani Tanga, Athumani Malunda, pichani.
Akizungumza mjini hapa, Mwenyekiti wa CCM wilayani Handeni, mkoani Tanga, Athuman Malunda, alisema kuwa wamejipanga kama chama kulinda heshima yao kwa kuongoza katika serikali za mitaa na vijiji.


Alisema kuwa ili watimize adhma yao, wataweka mfumo mzuri wa kuweka uongozi unaokubalika kwa wananchi wengi badala ya kupitisha mtu ambaye si chaguo la wananchi wao.


“Tumejipanga kupita kiasi kwa kuhakikisha kuwa chama kinashinda katika mitaa yote na vijiji vilivyopo katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga, ili pia iwe chachu ya kupatikana uongozi bora katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.


“Tukimaliza kupata wenyeviti wetu itakuwa njia nzuri ya kupata madiwani na mbunge pia, bila kusahau rais ambaye hapana shaka atatoka katika chama makini chenye dhamira ya kuwapatia maisha bora Watanzania wote,”alisema Malunda.


Wakazi wengi na wananchi wa Handeni wameendelea kuwa na imani na chama hicho kikongwe barani Afrika kutokana na kuwathamini katika chaguzi mbalimbali na kuwachagua wagombea wao kuanzia wenyeviti wa serikali za mitaa, vijiji, madiwani, mbunge na Rais pia.

No comments:

Post a Comment