Pages

Pages

Friday, January 17, 2014

Mbwana Matumla ajipanga vikali

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA wa ngumi za kulipwa hapa nchini, Mbwana Matumla, amesema anafanya juhudi kubwa ili kulinda jina na uwezo wake katika mchezo wa masumbwi nchini.

Bondia Mbwana Matumla, pichani.
Akizungumza hivi karibuni, jijini Dar es Salaam, Matumla alisema hali hiyo inatokana na mipango yake ya kuhakikisha kuwa jina lake halishuki katika tasnia hiyo.
Alisema ingawa amekuwa akipata matokeo mazuri ulingoni mara kwa mara, anaamini pia atafanikiwa kufanya vizuri kila atakapokwaana na mabondia mbalimbali ndani na nje ya nchi.
“Nimejipanga vizuri kulinda jina langu kwa kutambua namna ya kujiweka kwenye kiwango cha juu, ukizingatia kuwa huo ndio mpango mzuri wa kunipatia ushindi,” alisema.
Matumla ni miongoni mwa mabondia wenye makali ya kutisha, huku akitokea katika familia thabiti yenye historia ya mchezo huo wa masumbwi, wakiongozwa na kaka yao Rashid Matumla.

No comments:

Post a Comment