Pages

Pages

Friday, January 17, 2014

Malinzi: Soka la vijana wadogo ni muhimu

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
RAIS wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi, amesema kwamba kuna kila sababu ya kuweka mkazo kuweka program nzuri za kuendeleza soka la vijana ili iwe chachu ya kuendeleza mchezo huo.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi, pichani.
Akizungumza mapema wiki hii, Malinzi alisema kwamba juhudi za kuendeleza mpira wa miguu zitakwamua na kuleta mafanikio makubwa katika tasnia hiyo.
Alisema kuwa juhudi hizo pia zinaweza kwenda sambamba kwa kuanzia pia kwenye shule mbalimbali, ukizingatia kuwa huko ndipo kwenye watu wanaostahili kuanza kucheza soka.
"Hii itatusaidia kwa kiasi kikubwa kwakuwa ndio msingi imara wa kukuza sekta ya mpira wa miguu, ukizingatia kuwa ndio sera nzuri tunayohitaji kuisimamia kwa vitendo,” alisema.
Wakati anafanya kampeni za kumuingiza madarakani, rais Malinzi ilikuwa ni ajenda yake kubwa ya kuwa na ndoto ya soka la vijana, ikiwapo kuandaa mashindano ya vijana Barani Afrika, katika ardhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment