Pages

Pages

Sunday, January 05, 2014

Boban aripoti Coastal Union Tanga


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

KIUNGO mshambuliaji wa timu ya Coastal Union yenye maskani jijini Tanga, Haruna Moshi ‘Boban’, ameripoti mkoani Tanga kwa ajili ya kuanza mazoezi ya kujiandaa na mzunguuko wa pili wa ligi ya Tanzania Bara.

Haruna Moshi Boban pichani.
Kuripoti kwa Boban kunashusha presha kutoka kwa wadau wa timu hiyo wanaosema kuwa kiungo huyo amekuwa mtovu wa nidhamu kwa kuchelewa kuripoti kambini.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa timu ya Coastal Union, Hafidh Kido, alisema kuwa Boban aliafiki kujiunga na wenzake mapema wiki hii ili kuendelea na mazoezi ya pamoja.

Alisema kuwa kujiunga na wenzake katika maandalizi ya michuano ya Vodacom ni sehemu ya kujiweka sawa zaidi.

“Baada ya kumaliza ratiba yake kama alivyotoa taarifa kwa viongozi wake, Boban amejiunga na wenzake.

“Tunaamini mambo yatakuwa mazuri kwa kiungo huyo ambaye uwezo wake hapana shaka unajulikana na kuheshimika sana,” alisema.

Boban ni miongoni mwa wachezaji wanaoheshimika katika soka hapa nchini, huku uwezo wake ukiweza kufanya makubwa awapo uwanjani.

No comments:

Post a Comment