Pages

Pages

Saturday, January 18, 2014

CCM wilaya Kinondoni ilivyokutana mjini Bagamoyo kujenga chama chao, Mchumi wa Makumbusho, Yusuphed Mhandeni aongoza mashambulizi

Juzi mjini Bagamoyo mkoani Pwani kulifanyika Semina ya Wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Picha mbalimbali zikionyesha wana CCM hao katika semina hiyo. Mwenye kofia nyeusi ni Mwenyekiti wa CCM Kinondoni, Salum Madenge na nyuma yake mwenye shati la kitenge ni Mchumi wa Kata ya Makumbusho, Yusuph Mhandeni, maarufu kama Yusuphed Mhandeni, katika semina hiyo ya kujenga chama.

Mchumi wa Kata ya Makumbusho CCM, Yusuph Mhandeni, maarufu kama Yusuphed Mhandeni, akiwa na viongozi wa CCM wilaya Kinondoni, kwenye semina hiyo iliyofanyika wilayani Bagamoyo.
Baaada ya kumalizika semina, Yusuphed Mhandeni, alialikwa kwenye kutoa vyeti vya mafunzo ya mgambo wilayani Bagamoyo. Wanaoshuhudia meza kuu ni viongozi kutoka jeshi la Polisi..
 Wana CCM wakijiachia baada ya kumaliza semina hiyo wilayani Bagamoyo kwa ajili ya kuimarisha na kuijenga CCM kuelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment