Pages

Pages

Friday, November 08, 2013

Coastal yawaomba radhi mashabiki wao kwa kuvurunda mzunguuko wa kwanza wa ligi




Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KLABU ya Coastal Union yenye maskani yake jijini Tanga kwa Wagosi wa kaya, imewaomba radhi mashabiki wao kwa kumaliza vibaya mzunguuko wa kwanza wa ligi ya Tanzania Bara.
 
Hafidh Kido, Msemaji wa Coastal Union ya jijini Tanga, Tanzania.
Juzi katika Uwanja wa Chamazi uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam, Coastal walipigwa bao 1-0 dhdii ya timu ya JKT Ruvu, hivyo kumaliza ligi ikiwa na pointi 16.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Coastal Union, Hafidh Kido, alisema kwamba kitendo cha kumaliza vibaya kisiwaumize kichwa mashabiki wao.

“Tunawaomba mashabiki wetu wa kandanda wa Tanzania nzima kuendelea kuwa pamoja na sisi, tukiamini kuwa mzunguuko wa pili tutafanya vizuri katika ligi hii,” alisema.

Coastal ni miongoni mwa timu zilizokuwa zinapewa nafasi ya kufanya vyema katika patashika ya ligi ya Tanzania, ingawa imemaliza katika nafasi ya nane, ikiwa na pointi zake 16.

No comments:

Post a Comment