Pages

Pages

Saturday, November 09, 2013

Said Mbelwa na Kaoneka kupima uzito leo jijini Dar es Salaam


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

BONDIA Said Mbelwa 'Moto wa Gesi'  na mwenzake Shabani Kaoneka 'BSS' wanapima uzito leo Jumamosi kwa ajili ya pambano lao litakalofanyika Jumapili ya Novemba 10, Ukumbi wa Zulu Paradise, uliopo Pugu.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa pambano hilo, ambaye ni kocha wa mchezo wa masumbwi nchini, Rajabu Mhamila Super D, alisema kila kitu kimekamilika.

Alisema mabondia hao wanatakiwa wawe na kilo 76 kwa ajili ya kuingia ulingoni, huku tambo zikionekana kushika hatamu.

Mpambano wao utakuwa wa raundi 8, huku kukiwa na mabondia wa utangulizi, kama vile Hamza Mchanjo, Tony King, Chirambo Hemed, Sharifu Mzezele, Twalibu Mchanjo, Mohamed Kashinde, Adam Ngange na Shabani Mtengela 'Zunga Boy',” alisema Super D.
Kwa mujibu wa mratibu huyo, pia kutakuwa na uzinduzi wa DVD mpya za bondia Said Mbelwa alipocheza na nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment