Pages
▼
Pages
▼
Friday, November 08, 2013
Mwamtumu azikwa makaburi ya Mburahati, wenzake wamchangia 225,000
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MNENGUAJI wa bendi ya Extra Bongo, Mwantumu Athumani, amezikwa juzi jioni katika makaburi ya Mburahati, huku akihudhuriwa na watu mbalimbali waliosindikiza mwili huo.
Marehemu Mwantumu Athumani enzi za uhai wake.
Miongoni mwa watu waliokwenda kumzika marehemu Mwamtumu aliyewahi kufanya kazi na bendi kadhaa, ni Asha Baraka Mkurugenzi wa The African Stars, Twanga Pepeta na Ally Choki, ambaye ni bosi wa Extra Bongo.
Katika hali ya kuonyesha kuwa wadau wameguswa na msiba huo, Chama Cha Wacheza Shoo Tanzania, walitoa mchango wa Sh 225,000, chini ya Mwenyekiti wao mkoa wa Dar es Salaam, Super Nyamwela.
Katika mazungumzo jijini Dar es Salaam, Nyamwela alisema kuwa marehemu alikuwa mtu wa kujichanganya na watu, hivyo wamepoteza mtu muhimu.
“Japo huu ni mwanzo wa chama chetu, lakini tutaendelea kutumia muunganiko huu kwa kuishi kwa upendo na wadau wote, tukiwapo sisi wacheza shoo,” alisema.
No comments:
Post a Comment