Pages

Pages

Wednesday, October 02, 2013

Waziri wa Mambo ya Ndani Emmanuel Nchimbi, kuukwaa ubosi wa RECSA

Advera-Senso
                                                                                                                   
JESHI la Polisi kwa kupitia Msemaji wao Advera Senso pichani, limesema kuwa Tanzania inatarajia kupokea Uenyekiti wa Baraza la Mawaziri kwa Nchi za maziwa makuu na pembe ya Afrika katika mapambano ya kuzuia na kudhibiti uzagaaji wa silaha haramu (RECSA) kutoka nchi ya Rwanda.
 
Makabidhiano hayo yatafanyika kesho tarehe 03/10/2013 katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ya Rwanda atamkabidhi uenyekiti huo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Tanzania Mh.Dk Emmanuel Nchimbi.
 
Uenyekiti huo utadumu kwa muda wa miaka miwili ambapo katika kipindi hicho mikutano yote ya kukabiliana na uzagaaji wa silaha haramu itaratibiwa na Nchi ya Tanzania kupitia Jeshi la Polisi.

Umoja huo ulianzishwa mwaka 2005 kwa madhumuni ya kudhibiti uzagaaji wa silaha haramu kwa nchi za maziwa makuu na pembe ya Afrika ambazo ni pamoja na Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda na Tanzania.

   

No comments:

Post a Comment