Pages

Pages

Wednesday, October 02, 2013

Ngumi kutifuana katika pambano lingine la masumbwi Oktoba 26 mwaka huu, Ukumbi wa Panandi Panandi

Kocha wa Masumbwi nchini, Super D akitoa neno katika biashara yake ya kuuza cd za masumbwi.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MPAMBANO mwingine wa masumbwi unatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Panandi Panandi Oktoba 26 chini ya uratibu wa Kinyogoli Fondition, huku ukiwakutanisha mabondia mbalimbali.

Akizungumzia mchezo huo kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini kutoka kambi ya ilala Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mpambano huo utawakutanisha bondia Yakubu Maganga atakae zichapa na Ubwa Salumu katika uzito wa kilo 75 huku Seif Ali akipambana na Hassani Labanda pamoja na mipambano mengine ya masumbwi itakayo wakutanisha mabondia mbalimbali

Siku hiyo kutakuwa pia na huzwaji wa DVD kali za ngumi wakiwemo mabondia wakali wanaotamba Duniani na hapa nchini kama.Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar, Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi DVD hizo za ngumi kali zitakuwa zikiuzwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'

Pamoja na kutambua sheria na taratibu za mchezo huo siku hiyo pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo huo wa masumbwi vitakavyotolewa  zawadi kwa mabondia na Kocha Super D  ambaye ame haidi kutoa, Gum Shit ,Clip Bandeji,DVD za Mafunzo kwa mabondia, Bukta,Protector na vifaa mbalimbali kwa mabondia watakao onesha uwezo wa ali ya juu wa kutupiana masumbwi.

No comments:

Post a Comment