Pages

Pages

Tuesday, October 08, 2013

Wasajili wapya watano waapishwa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Fakih Jundu akimuapisha, Mhe. Dustan Ndunguru kuwa Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, kabla ya uteuzi wake Mhe. Ndunguru alikuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Mkoa Lindi.

Jaji Kiongozi Mhe. Fakih Jundu akimuapisha Mhe. William Mutaki kuwa Naibu Msajili Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kabla ya uteuzi wake Mhe. Mutaki alikuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Jiji.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Fakih Jundu akimpongeza Mhe. Francis Kabwe kwa shada la maua, Mhe. Jaji Kiongozi ameaapisha jumla ya Wahe. Watano walioteuliwa kuwa Wasajili katika ngazi za mbalimbali za Mahakama. (Picha na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania).

No comments:

Post a Comment