Pages

Pages

Tuesday, October 08, 2013

Hii ndio Hifadhi ya Taifa ya Saadani na jinsi inavyopendeza kuangalia vitu vingi vilivyomo ndani yake

Na Amina Omari, Pangani
HIFADHI ya Taifa ya Saadani ni moja kati ya hifadhi za Taifa 16 yenye
vivutio vingi vya kuvutia wageni kuona, kuburudika na kujifunza vitu
vilivyomo kwenye mbuga hiyo pamoja na kuchangia na kukuza pato la
Taifa kupitia sekta ya utalii nchini.

Hifadhi ya Taifa ya Saadani, inavyoonekana pichani.
Hifadhi hiyo imepandishwa hadhi na kuwa hifadhi kamili mwaka 2005
kutoka kuwa pori la akiba, ina aina ya upekee kwa sababu inapakana na
bahari ya Hindi unapotembelea unaweza kufanya utalii wa nchi
kavu, majini na kwenye maeneo ya historia ya mambo ya kale.

Hii ndio hifadhi ya Taifa Saadani, ukifika utajionea vitu vingi vinavyotia raha kwa kiasi kikubwa mno.

Hivi karibu Shirika la Hifadhi ya Taifa TANAPA lilitoa ufadhili kwa
chama cha waandishi wa habari za mazingira Mkoani Tanga, TARUJA kwa ajili ya kwenda kujifunza uandishi wa habari za mazingira na uhifadhi ikiwa na lengo la kuongeza weledi wa kuripoti habari hizo.

Mhifadhi Mkuu wa Saadani, Hassan Nguluma
Hivyo waliitumia hifahi hiyo kama sehemu yao ya mafunzo lakini ni kutoka na Kuwa  imezungukwa na wananchi kwa kiasi kikubwa  na kupaka na bahari huku jamii ya watu wa pwani wakitegemea bahari kama sehemu yao ya kitega uchumi nao wanyama wakiona bahari pia ni sehemu yao

Upekee mwingine unatoka na mwingiliano wa makazi ya wananchi  kutoka na hifahi hiyo kupakana na vijiji ,kuna maeneo ukitembea  kwa  umbali fulani unakutana na makazi  ya watu kisha mbele kuna hifadhi yenye wanyama wengi  na wakuvutia .

Pia katika hifadhi ya Saadani unaweza kufanya utalii wa kutumia boti kwenye mto wami kwenda umbali mrefu kuna ndege wengi na wanyama aina ya viboko na mamba ndani  na nje ya maji na kwenda hadi sehemu  bahari na mto vinapokutana huku kukiwa na miti aina ya mikoko kwa uwanda wa pwani.

Ndani ya Hifadhi kuna mazingira  yenye kuvutia huku upepo mwanana ukivuma kutoka bahari ya Hindi ukipuliza kwenye uneo la kubwa la hifahi hiyo,ofisi za hifadhi zimejengwa kwenye maeneo ya karibu na
makazi ya wananchi,katika ya hifadhi pamoja na mpakani.

Mhifadhi Mkuu wa Saadani, Hassan Nguluma, anasema hifadhi hiyo imebeba jina la kijiji cha Saadani ambacho  hapo awali lilikuwa ni eneo la historia lilianzishwa na wavuvi kwa ajili ya kupumzika wanapo kuja
kuvua katika pwani hiyo kwenye karne ya 19.

“Kutoka na eneo hilo kutokuwa na makazi wavuvi walikuwa wanapita kwa ajili ya kupumzika wakati wakiendelea na shughuli zao za uvuvi ndipo baadae wakaanzisha makazi ambayo kwa sasa pamekua ni hifadhi za wanyama na vivutio,”alisema Ngulume, akizungumza na Handeni Kwetu Blog, katika hifadhi hiyo.

Amesema kuwa hifadhi hiyo ipo kando kando ya bahari ya Hindi imepakana na mikoa ya Pwani na Tanga ambapo hifadhi ipo ndani ya Wilaya za Bagamoyo, Pangani na Handeni.

Vivutioa vya utalii vinavopatikana kwenye hifadhi hiyo ni pamoja na fukwe nzuri zenye uasili wake ,aina mbalimbali za wanyama na ndege huku kukilwa na zaidi ya iana 200 za ndege wakiwawo wanao hamahama
kutoka na misimu mbalimbali ya eneo hilo.

“Mazalio ya kasa,misitu ya mikoko na ile ya ukanda wa pwani,maeneo ya mabaki wa kihistoria pamoja na mila na desturi za tamaduni za wenyeji wa pwani ni baadhi tu ya vivutio vinavyopatika katika hifadhi hii ya
saadani,”alisema Mhifadhi mkuu huyo.

Shughuli za utalii zinaweza kufanyika kwa njia ya mitumbwi ,kutembea na gari,au kwa miguu hasa kwenye fukwe,kuangalia ndege aina mbalimbali na kutmelea kwa miguu kwenye msitu wa Zaraninge ambapo wenyeji
hufanya matambiko.

Licha ya uzuri wote huo pia utembeleapo  hifadhi ya saadani utakuta mabaki ya kihistoria ya kuonyesha kuwa eneo hilo liliwahi kutawaliwa na jamii ya watu wa Kiasia kwani kuna eneo la kwanza la soko la
watumwa lililipo kwenye kijiji cha Saadani.

Kuna makaburi ya wakoloni kuashiria kuwa wakoloni wa kijerumani nao waliwahi kuishi katika eneo hilo na eneo maarufu la kutolea adhabu ya kifo kwa waafrika mbuyu Nyonga ambao ukifika kwenye hifadhi hiyo
utakuta historia hiyo .

Kutoka na uwepo wa maeneo ya historika katika hifadhi hiyo SANAPA wamepanga kubuni miradi ya  vivutio vya asili vilivyoko kwenye vijii vya maeneo yanayozunguka hifadhi hiyo ili kuimarisha uchumi kwa jamii inayozunguka hifadhi hiyo kwa sasa.

Meneja Ujirani mwema Taifa Ahmed Mbagi  amesema miradi huyo ni sehemu ya mipango waliyokuwapo nayo ya kuhakikisha vijiji vinavyopakana na hifadhi za taifa kunufaika na wageni wanaoingia kwa ajili ya kujionea njia ya vivutio vya asili vilivyoko kwenye maeneo yao kwa lengo la kujiongeza kipato.

“Nia yetu ni kuona wanachi wananufaika na raslimali walizokuwapo nazo kwa kuweka utaratibu wa kila maeneo kutangaza vivutio walivyonavyo zaidi ya wanyama walioko kwenye hifadhi basi wajionee mila na tamaduni zilizoko sehemu husika," alisema Mbagi.

Nae Mtendaji wa Kijiji cha Saadani Hussein Mselo amesema kuwa bado wananchi wa maeneo hayo hawana muako wa kutangaza vivutio vilivyoko kutoka na kukosa uwelewa wa taratibu za uendeshaji wa vivutio hivyo.

“Hapa kijijini tuna vivutio kama soko la watumwa,mbuyu nyonga ambao ulitumika kuwanyonga watumwa pamoja na makaburi ya wajerumani wakwanza kufika saadani lakini kutoka na kukosa uwelewa wa kuvitangaza vivutio hivyo tunakosa fedha kutoka kwa watalii”alisema Mselo.

Alisema kwa sasa waandaa utaratibu wa kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi  wa maeneo ya jirani yenye vivutio hivyo ili kujua umuhimu wake pamoja na fursa zilizopo ili waweze kuiongezea kipato kitakacho
saidia kijiji na wananchi wake.

“Eneo hili la vivutio vya kale lipo chini ya kijiji lakini kutoka na kutokuwa na elimu sahihi ya maswala ya utalii wa mambo ya kale kijiji kimekuwa kikosa mapato na wananchi nao kama wamekata tamaa kutoka na kutegemea TANAPA kuwasidia kiuchumi,”alisema Mselo.

Pia aliongeza kuwa iwapo saadani ingewawezasha kifedha na elimu kuhusu matumizi ya raslimali hizo wangeweza kupata pato nzuri kwani watalii wanapokuja kuona wanyama wangeweza kutumia fursa hiyo kuona historia pia

Kwenye hifadhi hiyo kati ya wanyama watano mashuhuri wanaopatika kwenye mbuga kubwa  za hifadhi za taifa na ulimwenguni (Big five) wanne wanapatikana kwenye hifadhi ya Saadani ambao ni Tembo, Simba
Nyati, na Chui isipokuwa Faru pekeee ndio hapatikani.

Katika ya wanyama hao Tembo amekuwa ni kivutio kikubwa kwa wageni mbalimbali watembeleao kwenye hifadhi hiyo kutoka na maisha yake kulindana na binadamu anapokufa mmoja hukusanyana na kuomboleza sehemu mwezao alipofia na huwana tabia ya kurudi mara kwa mara kwenye eneo hilo na huzika kwa kufunika kwa majani ya miti na huwa wakali sana kipindi hicho.

Haya hivyo Mhifadhi mkuu anasema kuwa changamoto kubwa wanayokutana nnayo kwa sasa  ni jamii kutokubali  kufuata sheria kwa kufanya shughuli za kibinadamu kwenye hifadhi hiyo na wengine hupenda
kusaidiwa kibinafsi badala ya wote kwa ujumla



No comments:

Post a Comment