Pages

Pages

Sunday, October 13, 2013

Taarifa ya uhakika: Ufoo Saro apigwa risasi na mzazi mwenzake, mama yake afariki Dunia kwa kupigwa risasi



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWANDISHI wa ITV na Radio One, Ufuo Saro amepigwa amepigwa risasi ya tumbo na kwenye paja na sasa yupo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili akiendelea na matibabu huku hali yake ikiwa si ya kuridhisha.
Mwandishi wa ITV na Radio One, Ufoo Saro, pichani, aliyepigwa risasi, ambapo mama yake amefariki Dunia katika tukio hilo.

Katika tukio hilo, mama yake mzazi Saro, anayejulikana kwa jina la Anastazia Peter Saro naye alipigwa risasi ya kwenye matiti na kupelekea kifo chake papo hapo, katika tukio linalodaiwa kufanywa na na mtu anayejulikana kwa jina la Mushi ambaye pia alifariki kwa kujipiga risasi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura, aliuambia mtandao wetu wa Handeni Kwetu kuwa, kuwa uchunguzi wa awali unaendelea, huku Ufoo Saro mwenyewe akishindwa kuzungumzia suala kwakuwa yupo chini ya uangalizi ya madaktari Muhimbili.

Mushi anayefanya kazi UN nchini Sudan, aliwasili jana akitokea eneo lake la kazi ambapo enzi za uhai wake alizaa na Saro. Kamanda huyo anaendelea kusema kuwa, Mushi alifikia eneo la Mbezi Magari Saba, jijini Dar es Salaam, kabla ya leo saa 12:30 kufika kwa mkwe wake nyumbani kwa kina Saro.

Baada ya kufika hapo, alitoa bastola yake na kumpiga mkwe wake, mzazi mwenzake na kujimaliza mwenyewe, ambapo bado uchunguzi unaendelea kujua kiini cha sakata hilo.

“Taarifa hizi zitakamilika pale Ufo Saro atakapohojiwa na polisi kwakuwa yeye ndio mhusika kwakuwa nyumba ile ilikuwa na watu watatu, ambapo wawili kati yao ni marehemu.

“Tutaendelea kulifanyia kazi suala hili, ambapo sasa majeruhi yupo Muhimbili akipatiwa matibabu wakati miili ya marehemu pia imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali hiyo ya Taifa, Muhimbi,” alisema.

Watu mbalimbali katika mitandao ya kijamii wameonyesha kushangazwa na tukio hilo alilofanyiwa mwanadada huyo anayefanya kazi katika kituo cha ITV na Radio One, kinachomilikiwa na Kampuni ya IPP, chini ya Mwenyekiti wake Reginald Mengi.

No comments:

Post a Comment