Pages

Pages

Sunday, October 13, 2013

Kamati ya Gurumo 55 yajipanga upya


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

KAMATI inayoandaa namna ya kumuaga mwanamuziki mkongwe hapa nchini, Muhdini Gurumo, imesema inajipanga upya baada ya kushindwa kufanya tamasha la Gurumo 55 juzi Oktoba 11 kama walivyowatangazia Watanzania.

Mwenyekiti wa Kamati ya Gurumo 55 Asha Baraka akizungumza jambo kulia, akiafutiwa na Mzee Gurumo, Juma Mbizzo, Saidi Kibiriti katika moja ya matukio ya kutangaza tukio hilo ambalo kwa sasa limeota mbawa.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa bendi ya The African Stars Twanga Pepeta, Asha Baraka, alisema kuwa mchakato huo ulikabiliwa na matatizo mengi, yakiwakiwamo wadau wa kamati hiyo kubanwa na vitu vingine.


Alisema awali walipanga tamasha la kwanza lifanyike Oktoba 11 mwaka huu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, ila walishindwa kufanya hivyo kama walivyopanga.


Asha aliwatoa hofu Watanzania na wadau wa muziki kuwa tukio hilo litafanyika kama ilivyopangwa, japo haitakuwa kwa tarehe iliyowekwa hapo kabla.

“Katika matukio kama haya kunahitaji mipango mingi, hivyo litafanyika kama ilivyopangwa na kuhakikisha kuwa tunafanikisha dhamira zetu.


“Naamini siku chache zijazo tutangaza upya namna gani tutafanya kwa ajili ya kumuaga mwanamuziki Gurumo na kuweka mipango kabambe ya kuthamini mchango wake,” alisema Asha.


Kamati hiyo pia imekusanya watu kadhaa, akiwamo Mkurugenzi wa Screen Masters Said Mdoe, Juma Mbizo na wengineo waliokuwa na lengo moja la kufanikisha jambo hilo.

No comments:

Post a Comment