Pages

Pages

Friday, September 27, 2013

Watanzania waaswa wathamini ibada kwa ajili ya kumpendeza Mungu



Na Kambi Mbwana, Handeni
WAUMINI wa dini ya kiislamu na Watanzania kwa ujumla wameombwa washiriki katika ibada ili wajiwekee mazingira mazuri ya kumrudia Mungu na kuacha vitendo viovu.
Sheikhe wa Kijiji cha Komsala, Ramadhan Mavyombo, akizungumza jambo na watu waliohudhuria kumbukumbu ya mzee Mbwana Hemed, kijijini hapo juzi, wilayani Handeni, mkoani Tanga.

Hayo yamesemwa na Shaikhe wa Kijiji cha Komsala, wilayani Handeni, mkoani Tanga, Ramadhan Mavyombo katika shughuli ya kumbukumbu ya marehemu Mbwana Hemed, iliyofanyika kijijini hapo juzi Septemba 25 na kuhudhuriwa na watu wengi.

Akizungumza na Handeni Kwetu Blog, Mavyombo alisema kuwa mtu anayemjua Mungu kwa kushiriki katika ibada, kamwe hawezi kutenda vitendo viovu.

Alisema ni lazima Watanzania wote washiriki katika ibada maana ni njia nzuri ya kumrudia Mungu na kuwa wanadamu wema wenye kuweza kuifanya Dunia iwe sehemu nzuri ya kuishi.

“Jamani ndugu zangu Watanzania kwa imani mbalimbali, ni wazi tunapaswa kumrudia Mungu kwa kushiriki kwenye ibada na kuacha yale aliyoyakataza.

“Tukifanya hivyo, tutakuwa sehemu nzuri katika Dunia hii na siku tutakapotaangulia mbele ya haki, maana sote tutakufa hivyo lazima tuwe katika imani,” alisema.

Mzee Mbwana Hemed, maarufu kama Kajembe, alifariki ghafla mwaka jana na kuzua hofu kwa wananchi wa kijiji cha Komsala, wilayani Handeni mkoani Tanga kutokana na jinsi alivyoishi kwa upendo na ushirikiano na watu wote katika maeneo hayo.

No comments:

Post a Comment