Pages

Pages

Tuesday, September 24, 2013

Handeni sasa kujipanga na maabara shule za sekondari


Na Kambi Mbwana, Handeni
MKURUGENZI Mtendaji wilaya Handeni, mkoani Tanga, Khalfany Haule, amesema wanakabiriwa na changamoto ya ukosefu wa maabara kwa shule za sekondari, hivyo wanajipanga kushirikiana na wadau ili kufanyia kazi na kuinusuru elimu wilayani humo.



Mkurugenzi Mtendaji wilayani Handeni, Dr Khalfany Haule, pichani, akiwa ofisini kwake.

Akizungumza mjini hapa, Haule alisema maabara hizo ni kwa shule zote za sekondari zilizopo wilayani humo, jambo ambalo linaweza kuchangia kufanya vibaya kwa wanafunzi kwenye mitihani ya Taifa.
Alisema anajipanga na watendaji wengine wilayani humo, ikiwa ni sambamba naa kubuni wazo la kuwashirikisha watu wenye moyo na uwezo wao kulitatua suala hilo kwa kiasi kikubwa.

"Hapa kuna shule za sekondari ambazo kwa hakika zinafanya vibaya kwasababu ya ukosefu wa maabara za kuwapa wanafunzi mwanga wa kuendelea vyema katika masomo yao.


"Lengo ni kuanza kujenga maabara hizo, hivyo tutapenda kushirikiana na wadau wote wenye malengo ya kuinusuru elimu ya Tanzania kwa kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaandaliwa vyema,” alisema Haule.

Wilaya ya Handeni ipo chini ya Mkuu wa wilaya wake, Muhingo Rweyemamu, huku ikifanikiwa na kuwa na mbunge Abdallah Kigoda ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara.

No comments:

Post a Comment