Pages

Pages

Sunday, September 15, 2013

Ukosefu wa maji ya kutosha kwaumiza vichwa serikali wilayani Handeni, mkoani Tanga



Na Mwandishi Wetu, Handeni
KATIBU Tawala wa wilaya Handeni, mkoani Tanga, John Ticky, amesema kuwa endapo wilaya yao ingekuwa na maji ya kutosha au mvua za kueleweka, wakazi na wananchi wangekuwa matajiri.
Katibu Tawala, wilayani Handeni, mkoani Tanga, pichani.
Hiyo ni kutokana na ukubwa wa ardhi na iliyokuwa na rutuba kiasi cha kuwafanya watu waitumie kwa ajili ya kufanikisha maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza na Handeni Kwetu Blog hivi karibuni wilayani hapa, Ticky alisema kuwa siku zote Mungu hawezi kukupa vyote, hivyo endapo Handeni ingekuwa na maji ya kutosha wakazi wengi wangekuwa matajiri wa aina yake.

“Unaweza kushangaa kwanini watu wengi wanashindwa kujikimu licha ya kuwa na ardhi ya kutosha na yenye rutuba, ila wakati mwingine uhaba wa maji na mvua zisizokuwa na mpangilio unakwamisha.

“Endapo maji yangekuwa mengi kama ilivyokuwa kwa baadhi ya wilaya, wakazi na wananchi wa Handeni wangenufaika kwa kiasi kikubwa kwa kuitumia ardhi kwa kilimo na kuchangia katika maisha yao,” alisema Ticky, Katibu Tawala wilayani Handeni.

Wananchi wengi wa Handeni wanatumia kilimo kwa kutegemea mvua ya msimu kutokana na maeneo mengi kuwa na uhaba wa maji, hasa ukosefu wa mito ya kutiririsha maji.

No comments:

Post a Comment