Pages

Pages

Sunday, September 15, 2013

Simba, Mtibwa zaingiza Milioni 95 baada ya kuingia watazamaji 16,507

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Mtibwa Sugar iliyochezwa jana (Septemba 14 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza Sh. 95,080,000.

Rais wa TFF, Leodgar Tenga, pichani.
Msemaji wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema kuwa watazamaji 16,507 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 15 ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa wenyeji Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.


Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 23,018,077.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 14,503,728.81.


Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 11,704,107.18, tiketi sh. 2,548,890, gharama za mechi sh. 7,022,464.31, Kamati ya Ligi sh. 7,022,464.31, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,511,232.15 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,730,958.34.

No comments:

Post a Comment