Pages

Pages

Sunday, September 15, 2013

Mchumi wa CCM Kata ya Makumbusho aonja utamu wa lami wilayani Handeni na kuimwagia sifa serikali



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MCHUMI wa Kata ya Makumbusho wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mdau wa muziki wa dansi hapa Tanzania, Yusuph Mhandeni, ameipongeza serikali kwa kutengeneza barabara mbili za Korogwe Handeni na Handeni Mkata kwa kiwango cha lami.
Yusuphed Mhandeni akiwa Kwachaga, wilayani Handeni leo wakati anarudi jijini Dar es Salaam, akitokea mkoani Kilimanjaro.

Wakati barabara ya Mkata hadi Handeni mjini ikiwa imeshakamilika, ile Handeni hadi Korogwe inaelekea mwishoni, jambo linaloweza kuleta maendeleo wilayani humo na Tanzania kwa ujumla.
Yusuphed Mhandeni, nyuma, akiwa kwenye matukio ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kutoka wilayani Handeni, akitokea mkoani Kilimanjaro, ambapo aliamua kupitia wilayani Handeni, Mhandeni alisema anayesema Handeni hakuna maendeleo ana lake jambo.

Alisema kuwa barabara hizo za kiwango cha lami kumerahisisha maisha, ukizingatia kuwa ni rahisi pia mtu anayetoka Arusha akaingilia Handeni hadi Mkata, ikiwa ana lengo la kuja jijini Dar es Salaam.

Awali, Mhandeni aliandika kwenye group (forum) lilipo kwenye mtandao wa kijamii (facebook) ambalo ni ndugu na blog hii, inayoitwa pia kwa jina la Handeni Kwetu, akizungumzia safari yake na jinsi alivyofurahia uwapo wa barabara hizo.

“Haya ni mafanikio makubwa kwa serikali ya CCM katika kuhakikisha kuwa barabara hizi zimekamilika zote kwa kiwango cha lami na kuyafanya maisha yawe rahisi.

“Wanaosema Handeni hakuna maendeleo wanapaswa waangalie pia kupatikana kwa barabara hizi maana ni njia ya kuwafanya wananchi wajimudu kiuchumi hasa kwa wale wafanyabiashara wanaoingia na kutoka katika wilaya ile,” alisema Mhandeni.

Mara baada ya kufika wilayani Korogwe, Mhandeni alivipita vijiji vya Komsala, Kwamatuku, Sindeni, Misima, Kwenjugo na Handeni mjini, kabla ya kuelekea tena Mkata na kushika njia ya kuelekea jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment