Pages

Pages

Tuesday, September 24, 2013

Tamasha la Utamaduni Handeni Kwetu kufanyika Desemba 14 mwaka huu wilayani Handeni, mkoani Tanga


Na Mwandishi Wetu, Handeni
TAMASHA la Utamaduni lililopewa jina la ‘Handeni Kwetu 2013’ linatarajiwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu wilayani Handeni, mkoani Tanga, likiwa na lengo la kutangaza sekta ya utalii na utamaduni wilayani humo.



 Mratibu wa Tamasha la Handeni Kwetu 2013, Kambi Mbwana, ambaye pia ni Mmiliki wa mtandao huu wa Handeni Kwetu Blog, pichani.



Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya Handeni, Dr Khalfany Haule, akizungumza na Handeni Kwetu, ofisini kwake muda mchache baada ya kuruhusu Tamasha la Handeni Kwetu kufanyika wilayani humo, Desemba 14 mwaka huu.



Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, akizungumza na Handeni Kwetu Blog, jana ofisini kwake wilayani Handeni, mkoani Tanga.

Handeni Kwetu linafanyika kwa mara ya kwanza tangu kuasisiwa kwa wilaya hiyo inayoongozwa kwa sasa na Mkuu wa wilaya Muhingo Rweyemamu.

Akizungumza jana wilayani Handeni, Mratibu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema wameamua kuandaa tamasha hilo ili kushirikiana na wadau wote kutangza utamaduni nchini Tanzania.

Alisema kadri siku zinavyozidi kusonga mbele, jamii nyingi zimekuwa zikiiga tamaduni za watu hasa kutoka nje ya nchi, jambo linaloleta mkanganyiko wa kiasi kikubwa.

“Tumeamua kuandaa tamasha hili kwa kupitia kampuni ya Raha Company and Entertainment, ambapo lengo kubwa ni kuhakikisha kuwa linafanyika kwa mafanikio makubwa.

“Mipango kabambe inawekwa kulifanya tamasha letu liwe na mguso wa aina yake, ukizingatia kuwa linafanyika mwishoni mwa mwaka, hivyo tunaamini watu wengi watashiriki na sisi, hasa wale waliokuwa kwenye kipindi cha mapumziko ya mwisho wa mwaka,” alisema Mbwana.

Mbali na kufanya tamasha la Utamaduni wilayani humo, pia kutafanyika mchezo wa riadha kwa ajili ya kuzindua hamasa katika mchezo huo wilayani Handeni, mkoani Tanga.



No comments:

Post a Comment