Pages

Pages

Tuesday, September 24, 2013

Maandalizi ya kumbukumbu ya baba yetu mzee Mbwana Hemed Masudi, yakiendelea kwa watoto kutembelea kwenye kaburi na kumuombea dua njema

Mama mzazi, Fatuma Rashid, akiomba dua ya marehemu mume wake, ikiwa ni maandalizi ya kumbukumbu ya mzee Mbwana Hemed Masudi, katika makaburi yaliyopo kijijini Komsala, wilayani Handeni mkoani Tanga.
Zaina Rajabu, akimuombea dua marehemu Mbwana Hemed Masudi katika kaburi lake, ikiwa ni maandalizi ya kumfanyia kumbukumbu ya mwaka mmoja baada ya kifo chake.
 Amina Rajabu, mjomba mtu akishiriki katika dua hiyo leo.
 Rashid Mbwana, akimuombea baba yake mzee Mbwana.
Kambi Mbwana kushoto na mchumba ake Grace Misango wakishiriki kwa pamoja katika dua hiyo ya kumuombea mema mzee Mbwana Hemed Masudi, leo kijijini kwao Komsala, wiilayani Handeni, mkoani Tanga.
Fatuma Omari Kadili, mwenye bai bui nyeusi akimuombea dua marehemu babu yake, mzee Mbwana Hemed Masudi katika maandalizi ya kumbukumbu yake itakayofanyika kesho, Komsala, wilayani Handeni mkoani Tanga.
Watoto na wajukuu wakiwa wamezunguuka kaburi la mzee Mbwana Hemed Masudi leo walipotembelea katika makazi yake ya milele.

No comments:

Post a Comment