Pages

Pages

Thursday, September 12, 2013

Miliki Biashara yako yachengua wengi Kimara Mwisho



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WADAU wa masuala ya burudani jana walijitokeza kwa wingi maeneo ya Kimara ya Mwisho katika tukio la kukabidhi bajaj tano za wateja wa Tigo, waliojishindia zawadi hizo kutoka katika Promosheni ya Miliki Biashara yako.

Ni tofauti maeneo mengine ya jiji ambapo wadau walionekana kuwa wagumu kucheza sebene, ila Kimara Mwisho walishikwa na hamasa ya aina yake.

Akizungumza katika makabidhiano ya bajaj hizo jana, Meneja Uzalishaji wa Kampuni ya Simu za Mikononi ya Tigo, Husni Seif, alisema kuwa wateja hao wamepewa bajaj baada ya kujishindia kutoka kwenye promosheni yao ya Miliki Biashara yako.

Alisema kuwa wanaamini wataendelea kuwa karibu na wananchi, hususan wale wataje wao kwa kuweka salio kuanzia sh 1000 ili wajipatie zawadi zao.

“Wateja ambao leo jana tumewakabidhi bajaj zao ni pamoja na Elinaza Fredrick Mbaruku, Godwin Angomisye Kajala, Meshack Abebe Ndoje, Judith Edmund Wilia na Adam Msafiri Arengo.

“Wateja wawili ambao ni Omari Mohamed Loya na Mohamed Simo Kirasa wao walikuwa na dharula, ila bajaj zao zipo watapewa wakati wowote kuanzia sasa,” alisema Seif mbele ya watu kibao waliohudhuria tukio hilo.

Kabla ya kuingia kwenye tukio hilo la kukabidhi bajaj za Tigo, wateja walipata fursa ya kuangalia vijana kadhaa waliopanda jukwaani kucheza muziki sanjari na kushiriki katika kujibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa.

No comments:

Post a Comment