Pages

Pages

Thursday, September 12, 2013

Diamond: Bado sijafika ninapohitaji ndio kwanza ninaanza



Na Kambi  Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul, maarufu kama Diamond, amesema licha ya kuonekana ni mwenye mafanikio katika tasnia hiyo, ila kwake ndio kwanza anaanza, hivyo kasi yake itaongezeka mara dufu.
Diamond pichani.
Diamond alishangaza wengi katika kutambulisha video ya wimbo wake My Number One, ambapo pia alimkabidhi gari mwanamuziki mkongwe Muhdin Gurumo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Diamond alisema kwamba wapo wanaoamini yeye ni mkali, ila bado ana safari ndefu ya kufanikiwa zaidi.

Alisema hali hiyo inamfanya aongeze kasi katika kutafuta nafasi ya kuwika zaidi kwa kutoa nyimbo nzuri sanjari na kujipatia mafanikio makubwa zaidi.

“Hii ni nafasi nzuri kwangu kusoma mchezo na kuongeza vionjo katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya, maarufu kama Bongo Fleva ili niwe juu zaidi.

“Bado sipo juu zaidi, hivyo nilipokuwa sasa nataka nifike mbali zaidi ili mambo yangu yawe mazuri zaidi katika tasnia hiyo ya muziki wa Bongo Fleva,” alisema.

Wimbo wa My Number One umeanza kujizolea umaarufu mkubwa kwa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya, ambapo ndani ya wimbo huo ametumia mtindo unaofahamika kama Ngololo na kugusa wengi.

No comments:

Post a Comment