Pages

Pages

Saturday, September 14, 2013

Cosmas Chidumule aurudia muziki wa kidunia na kuacha wokovu kwa ajili ya kumbeba mzee Gurumo



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWANAMUZIKI mkongwe hapa nchini, Cosmas Chidumule, amesema japo kuwa ameokoka, lakini atapanda jukwaani kuimba pamoja na mzee Muhidini Gurumo, katika shoo ya kumuaga iliyopangwa kufanyika Oktoba 11 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee na ile ya Novemba Mosi, TCC Sigara Chang’ombe.
Cosmas Chidumule kushoto akiwa na mzee Muhdini Gurumo.
Shoo hiyo imeandaliwa maalum kwa ajili ya kumuaga kiheshima mkali huyo aliyestaafu akiwa na bendi ya Msondo Ngoma inayotesa katika tasnia ya muziki wa dansi nchini.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Chidumule aliyeachana na muziki wa kidunia na kumrudia Mungu, alisema amezungumza na viongozi wake wa dini kwa ajili ya kuomba ruhusa ya kuimbaa jukwaani na Gurumo aliyechangia mafanikio yake.

Alisema kuwa hata biblia inawataka watu walie na wale wanaolia, hivyo haoni sababu ya kushindwa kupanda jukwaani kuimba pamoja na mzee Gurumo aliyeachana na muziki wa dansi kwa sasa.

"Nimeguswa vikali na maneno ya mzee wangu Gurumo aliposema amestaafu muziki huku akiwa hana baiskeli, hivyo nimeamua nishiriki katika shoo hii kwa ajili yake.

“Nadhani nitafanikisha kumpatia mwangaza wake mpya wa kimaisha, baada ya shoo hizo mbili, ukizingatia kuwa mzee anahitaji pesa na sio karatasi nje ya maisha ya kimuziki,” alisema.

Mbali na kupanga kuimba pamoja na Gurumo, Chidumule pia ni mjumbe wa Kamati iliyoundwa na kufahamika kama Gurumo 53, ikiwa na mipango kabambe kwa ajili ya kumtafutia chochote kitu, ikiwa ni pamoja na kuuza CD zake.

No comments:

Post a Comment