Pages

Pages

Wednesday, August 07, 2013

Yanga kwazidi kufukuta baada ya Manji kuitisha mkutano wa dharula

UONGOZI wa klabu ya Yanga, chini ya mwenyekiti wao Yusuf Manji, umeitisha Mkutano Mkuu wa dharula uliopangwa kufanyika Agosti 18 mwaka huu, katika Ukumbi wa PTA Sabasaba, jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto.
Ajenda kuu katika mkutano huo ni kutafakari kwa kina namna ya kuiweka Yanga yenye ushindi sambamba na maazimio ya kuonyesha mechi katika Kampuni ya Azam TV, kampuni wanayosema ni ndogo haiwezi kupewa jukumu la kuonyesha mechi hizo.

Pia Yanga wanasema Azam imepewa haki hiyo bila kugombania tenda kama inavyojulikana, jambo ambalo linaweza kuibua mkanganyiko wa aina yake katika soka la Tanzania.

Mkutano huo ni mwendelezo wa msuguano kutoka kwa Yanga wanaosita mechi zao kuonyeshwa kwenye Azam tv, huku wenyewe wakisema kuwa wapo watu wanaoshinikiza suala hilo.



No comments:

Post a Comment