Pages

Pages

Wednesday, August 07, 2013

Washindi saba wajishindia zawadi za bajaj kutoka Kampuni ya Tigo Tanzania

 Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga (kulia) akimkabidhi ufunguo wa Bajaji mshindi wa droo ya tatu wa promosheni ya Tigo ‘Miliki Biashara Yako’ Khalid Shabani katika hafla iliyofanyika Soko la Nyuki, Tegeta jijini Dar es Salaam.
 Washindi wa  droo ya tatu ya Tigo ‘Miliki Biashara Yako’ wakipozi mbele ya Bajaji zao walizokabidhiwa na kampuni ya simu ya Tigo katika hafla iliyofanyika Soko la Nyuki, Tegeta jijini Dar es Salaam.
 Mshindi wa promosheni ya Tigo ‘Miliki Biashara Yako’ Bw. Sande Juma (kushoto) akipokea ufunguo wake wa Bajaji kwa furaha kutoka kwa Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga katika hafla iliyofanyika Soko la Nyuki, Tegeta jijini Dar es Salaam.

 Washindi wa droo ya tatu wa promosheni ya Tigo ‘Miliki Biashara Yako’ (kutoka kushoto) Bw. Sande Juma, Tito Mkude  na Iddi Zonki wakikagua Bajaji walizokabidhiwa kutoka kwa kampuni hiyo ya simu katika hafla iliyofanyika Soko la Nyuki, Tegeta jijini Dar es Salaam.
 Washindi wa promosheni ya Tigo 'Miliki Biashara Yako' wakijaribu kwa furaha moja ya Bajaji zilizokabidhiwa na kampuni ya simu ya Tigo katika hafla iliyofanyika Soko la Nyuki, Tegeta jijini Dar es Salaam.

Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga akihojiwa na Waandishi wa Habari katika hafla ya makabidhiano ya washindi wa promosheni 'Miliki Biashara Yako' iliyofanyika Soko la Nyuki, Tegeta jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment